Tuesday, December 27, 2011

UWAZI: UGOMVI NA MKEWE, AUA WANAWE 2!



Jean Francis Say, 62, raia wa Ivory Coast, amewakaba koo na kuwaua watoto wake wawili, chanzo kikidaiwa ni hasira za kuachwa na mkewe, Adjoua ‘Antoinette’, 44.

Say, anadaiwa kuwaua watoto wake, mkubwa wa kiume, Rolls, 10 na mdogo wake wa kike, Regina mwenye umri wa miaka nane.

Wanandoa hao, wote wana asili ya Afrika Magharibi na walihamia London, England kwa ajili ya kusaka mafanikio zaidi ya kimaisha.

Say, alitenda unyama huo, kwenye makazi yake, Southwark, Kusini Mashariki ya London, na baada ya kumaliza, alimpigia simu mkewe aende kuchukua maiti.

Inaelezwa kuwa miezi sita kabla ya tukio hilo, Say aligombana na Antoinette ambaye aliondoka na watoto wake.

Inabainishwa kuwa siku ya tukio, Say baada ya kufanikiwa kukutana na wanaye, alikwenda nao Southwark ambako aliwafanyia unyama huo.

Habari zaidi zinaeleza kuwa katika simu aliyompigia Antoinette, alimueleza kuwa aongozane na polisi kwenda kuchukua maiti.

Antoinette, akiwa na polisi, walifika nyumbani kwa Say ambaye walimkuta amekaa jirani ni miili ya Rolls na Regina.

Say alifunga ndoa na Antoinette Februari 1998 kabla ya kuingia kwenye mtafaruku baada ya kutimiza miaka 12 ya ndoa.


Na Gazeti la Uwazi

No comments:

Post a Comment