Thursday, December 22, 2011

WATU 20 WALIOPATA UMAARUFU 2011

Shukrani kwa mwaka 2011, haukuwa mbaya kwa baadhi ya watu ambao hawakuwa na majina makubwa katika fani mbalimbali, lakini sasa angalau ukimtaja, anajulikana katika ulimwengu wa mastaa Bongo, Amani lina ripoti kamili.
Gazeti hili linakuletea listi ya majina 20 ambayo hata kama yalisikika huko nyuma, lakini mwaka 2011 uliowatoa kimasomaso.

AGNESS GERALD ‘MASOGANGE’
Huko nyuma aliuza nyago kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva kama Masogange ya Abednego Damian ‘Bele 9’ na kupewa jina la Masogange akibebwa na umbo lake ‘sexy’, lakini mwaka huu aliwika zaidi baada ya kujikita kwenye filamu za Kibongo.

HUSEIN MKIETY ‘SHARO MILIONEA’
Huku akiua ndege wawili kwa jina moja, jamaa kutoka Tanga ‘ali-hit’ kupitia uigizaji na muziki hivyo saluti kwa mwaka 2011.

MUVI ZA KIBONGO ZAWATOA WENGI
Wengi ambao sasa ni maarufu kutokana na ushiriki wao katika muvi za Kibongo kwa kucheza baadhi ya vipande au mhusika mkuu ni pamoja na Salma Jabu ‘Nisha’, Skyner Ally ‘Skaina’, Irene Paul na wengine kibao.

BONGO FLEVA HAIKUWA NYUMA
Kwa upande wa Bongo Fleva, majina mengi yalisikika, lakini yaliyotengeza vichwa vya habari ni pamoja na Aslay Isihaka ‘Dogo Aslay’, rais wa Darstamina, Nurdin Bilal ‘Shetta’, zao la Nyumba ya Kukuza Vipaji Bongo (THT), Ben Poul (alitwaa tuzo ya Kili 2011), Emmanuel Simwinga ‘Izzo Business’, Golden Mbunda ‘Godzillah’ na Ally Timbulo.

SHUKURANI KWA BSS 2011
Shindano la kusaka vipaji vya muziki la Bongo Star Search ‘Second Chance’ 2011, nalo lilitengeneza ‘kichwa’ kimoja, Haji Ramadhan aliyeibuka kidedea akiwaacha Rogers Lucas na Waziri Salum.

MNENGUAJI OTILIA
Kwenye unenguaji yalizoeleka majina ya akina Aisha Madinda, lakini mwaka 2011, jina la mnenguaji Otilia Boniface lilikua ghafla huku akihama kutoka Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’ na kutua Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’.

MARTHA MWAIPAJA
Muzuki wa Injili ulimpa jina Martha Esau Mwaipaja ambaye alitwaa tuzo ya Msanii Bora wa Kike Chipukizi 2011. Nyimbo zake za Tusikate Tamaa na Kwa Msaada Tutashinda kupitia albamu yake ya Tusikate Tamaa.

SALHA ISRAEL NA HUSNA MAULID
Kwenye urembo, Shindano la Miss Tanzania 2011 lilimtoa Salha Israel aliyeibuka kidedea huku mshiriki wake, Husna Maulid akikwaa skendo za mapenzi na picha za utupu hivyo kujitengenezea jina.

WATANGAZAJI
Majina ya watu mbalimbali yalisikika redioni na kuonekana runingani, hayakuchukua muda kukaa masikioni mwa wadau.
Baadhi yao ni pamoja na Jabir Saleh na Dj Cobo wa Times FM, Suddy Brown ‘Gosssip Cop’, Wasiwasi Mwabulambo, Raymond Mshana, Doreen Andrew na Mbwiga Mwigane, wote wa Clouds FM na Sayder Khalfan ‘Shadee’ wa Clouds TV.

BABU WA LOLIONDO
Mwanzoni mwa mwaka huu, Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Ambilikile Masapila ‘Babu wa Loliondo’ (pichani) alijizolea umaarufu kufuatia tiba yake ya kikombe kwa magonjwa sugu yakiwemo ukimwi, kisukari na presha aliyokuwa akitoa huko Loliondo, Arusha kabla ya baadaye kuibuka madai kuwa tiba hiyo haiponyi.


Na Sifael Paul, GPL

No comments:

Post a Comment