Monday, July 11, 2011

Ubunifu wa ANN LUKINDO wakimbiza UK

Kutoka kushoto: Marium Kilumanga, Jestina George, Anna Shelukindo
na mdau wakila pozi.



Mtanzania mbunifu wa mitindo ya nguo, Anna Lukindo, ametikisa ulimwengu wa fashion jijini london wikiendi iliopita. Anna alionyesha mavazi aliyobuni kwenye maonyesho ya La Geneve North Event, yaliyofanyika London siku ya Ijumaa tarehe 8.7.11 Ubunifu wa Anna ulipokelewa kwa vifijo na nderemo kwani ulikuwa ndio uliotia fora.

Kulikuwa na wabunifu wengine kumi, lakini Anna ndiye alikuwa mwafrika na Mtanzania pekee ambaye mavazi yake yalikubalika na kupendwa na watu wengi zaidi.

Mojawapo ya wageni na wadau mbalimbali walijjitokeza kumpa sapoti Anna ni Mh. Balozi wetu Peter Kallaghe na Mama Balozi, Naibu Balozi Chabaka Kilumanga pamoja na watanzania wengine.

Kwa niaba ya URBAN PULSE, tunapenda Kumpongeza Dada yetu Anna Na Kumtakia kila la kheri pamoja na Mafaniko Mema.


Kwa mawasiliano zaidi na Anna tembelea:

Pr/Media:Pauladpope@yahoo.co.uk
Web:www.annaluks.com
Twitter:@AnnaLukindo

imeletwa kwenu na:

URBAN PULSE CREATIVE
Urbanpulsecreative@googlemail.com

No comments:

Post a Comment