Monday, July 11, 2011

Christopher Brian Bridges a.k.a LUDACRIS ndani ya Dar

Mwanamuziki mahiri wa miondoko ya Hip hop ambaye pia ni muigizaji wa Filamu kutoka nchini Marekani ajulikanae kwa jina la Christopher Brian Bridges aliyezaliwa mnamo Septemba 11, 1977,ambaye pia anajulikana zaidi kwa jina la kisanii kama Ludacris, anatarajiwa kushuka nchini Tanzania na kuangusha bonge la shoo kwenye tamasha la miaka kumi ya msimu wa dhahabu unaoendelea na serengeti Fiesta 2011.

Akizungumza na kuthibitisha ujio wa Mwanamuziki huyo mapema leo asubuhi jijini Dar,Mkurugenzi wa Maendeleo na Utafiti wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba amesema kuwa,Mwanamuziki Ludacriss na mwanamuziki mwingine wa kimataifa kutoka nje (atatajwa hapo baadaye),wanatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha la miaka kumi ya msimu wa dhahabu unaoendelea na serengeti Fiesta 2011 kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar Es Salaam mnamo Julai 30.

No comments:

Post a Comment