Kikosi cha Young Africans kilichoanza katika mchezo wa Robo Fainali dhidi ya Mafunzo,na kuitoa kwa kwa mikwaju ya penati 5-3
Wachezaji wa timu zote, Young Africans na Mafunzo wakimpepea mchezaji Juma Othman Mmanga mara baada ya kuzimia, kabla ya kupata huduma ya kwanza na kuzinduka
Haruna Niyonzima, Athuman Idd Chuji, Jeryson Tegete wakishangilia ushindi, mara baada ya Chuji kufunga penati ya mwisho na ya Ushindi
***
Young Africans Sports Club mabingwa watetezi wa kombe la Kagame, wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu failnali mara baada ya kuifunga timu ya Mafunzo FC kutoka Zanzibar jumla ya penati 5-3, kufuatia kwenda sare ya kufungana bao 1 -1 katika dakika 90 za mchezo.
Mchezo huo uliofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ulianza majira ya saa 10 jioni ukiwa ni mchezo wa pili baada ya mchezo wa kwanza uliotangulia kati ya APR ya Rwanda iliyoifunga URA ya Uganda jumla ya mabao 2-1.
Mchezo ulianza kwa kasi toka dakika ya kwanza ya mchezo, kwa wachezaji wa timu zote kuonyesha umahiri wa kuumiliki mpira, na timu ya Mafunzo ilionekana kukamia mchezo huo kwani wachzaji wake walijituma sana kuhakikisha wanapata bao la mapema.
Mpaka dakika 30 za mchezo timu zote zilikuwa hazijafungana, Mafunzo ilitumia mchezo wa kujaza viungo wengi katikati na kufanikiwa kuimiliki sehemu ya kiungo, kwani katika dakika ya 34, Mafunzo ilijipatia bao lake la kwanza kupitia kwa mfungaji All Othman Mmanga aliyefunga kwa kichwa krosi iliyopigwa na kiungo wa timu hiyo.
Mpaka timu zinakwenda mapumziko, Mafunzo walikuw ambele kwa bao 1- 0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa Young Africans kufanya shambulizi la kushitukiza, ambapo katika dakika ya 46, Mshambuliaji Said Bahanunzi aliipatia Young Africans bao la kusawazisha kwa kichwa akiunganisha krosi ya beki wa kulia Juma Abdul.
Kuona hivyo Mafunzo waliamka na kuanza kulishambulia lango la Young Africans lakini umahiri wa walinzi wa Young Africans ulikuwa kikwazo kwao kushindwa kumfikia mlinda mlango Yaw Berko.
Young Africans ilifanya mabadiliko ya kuwatoa Yaw Berko aliyeumia na nafasi kuchukuliwa na Ally Mustapha 'Barthez', Jeryson Tegete aliyechuku anafasi ya Rashid Gumbo na Idrisa Rashid aliyechukua nafasi ya Stephano Mwasika, mabadiliko ambayo hayakubadili matokeo.
Dakika ya 80, mchezo ulismama kwa dakika zipatazo 5 kufuatia mchezaji wa Mafunzo Juma Mmanga kupoteza fahamu na wachezaji wa timu zote kuvua jzei zao na kuanza kumpepea, huku wengine wakiangua vilio kabla Daktari wa Young Africans Dr.Suphian Juma kwenda kumsaidia na kumzindua kisha kutolewa nje kwa machela na kwenda kupewa matibabu zaid katika gari la wagonjwa la dharula.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 1 - 1 Mafunzo, hatua iliyopelekea kupigwa kwa mikwaju ya penati.
Waliofunga penati kwa upande wa Young Africans ni: Said Bahanunzi, Nadir Haroub Cannavaro, Hamis Kiiza na Athuman Idd Chuji
Huku Mafunzo wakipata penati 3, huku Said Musa Shaban akitoa moja nje ya lango penati yake na Young Africans kufuzu hatua ya nusu fainali kwa jumla ya penati 5-3.
Kwa matokeo hayo, Young Africans itacheza na APR ya Rwanda katika mchezo wa NUSU FAINALI.
Young Africans; Yaw Berko/Ally Mustafa, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Rashid Gumbo/Jeryson Tegete, Haruna Niyonzima, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza, Stephano Mwasika/Idrisa Rashid
Mafunzo FC; Khalid Mahadhi Hajji, Ismail Khamis Amour/Hajji Abdi Hassan, Said Mussa Shaaban, Salum Said Shebe, Ali Othman Mmanga, Juma Othman Mmanga/Sadik Habib Rajab, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Jaku Juma Jaku, Mohamed Abdulrahim, Wahid Ibrahim/Kheir Salum Kheir na Ally Juma Hassan.
(picha na www.bongostaz.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment