Kikosi cha Young Africans kilichoichapa APR mabao 2 - 0, katika mchezo wa kundi C wa mashindano ya kombe la Kagame yanayoendelea jijini Dar es salaam
Said Bahanunzi akishangilia na Hamis Kiiza mara baada ya kufunga bao pili. Bahanunzi alifunga mabao yote 2 katika mchezo dhidiya APR
***
Mabingwa watetezi wa kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (KAGAME) timu ya Young Africans Sports Club imeichapa timu ya APR kutoka Rwanda mabo 2 - 0 katika mchezo wa mwisho wa kundi C uliofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Young Africans iiliyoingia uwanjani kupigana kuhakikisha inapata ushindo katika mchezo huo, ilianz akwa kufanya mashambulizi langomi mwa APR mwanzoni mwa mchezo tu, na kama washambuliaji wake wangekuwa makini wangeweza kupata mabao ya mapema.
Dakika ya 22 ya mchezo mshambuliaji Said Bahanunzi aliipatia Young Africans bao la kwanza, mara baada ya kumalizia pasi safi iliyopigwa na mshambuliaji Hamis Kiiza aliyewatoka walinzi wa APR na kupiga krosi hiyo iliyomkuta mfungaji aliyeukwamisha wavuni bila ajizi, na kumuacha mlinda mlango wa APR Jean Claude Ndoli akiruka bila mafanikio.
kufungwa bao hilo, iliamka na kucheza mpira wa pasi fupi fupi, kitu kilichowapeleka kuutawala mchezo na kuwanyima fursa viungo wa Young Africans kushindwa kumiliki eneo la katikakti lakini umakini wa walizni wa Young Africans ulikuwa kikwazo kwa washambuliaji wa APR
Dakika ya 42 ya mchezo, Said Bahanunzi aliukwamisha wavuni mpira, lajkini mwamuzi wa mchezo alilikataa bao hilo kitu kilicholeta kelele nyingi kwa washabiki na wapenzi waliokuwepo uwanjani, wakimlaumu kwa kulikataa bao hilo safi.
Mpaka mpira unakwenda mapumziko, Young Africans ilikuwa mbele kwa mabao 1- 0.
Kipindi cha pilik kilianza kwa Young Africans kufanya mabadiliko ambapo iliwapumzisha Nizar Khalfan,nafasi yake ikachukuliwa na Juma Seif Kijiko, mabadiliko hayo yaliendelea kuisaidia Young Africans kwani waliendelea kuwabana APR na kukosa nafasi ya kumfikia mlinda mlango Yaw Berko aliyekuwa likizo kwa mda mrefu wa mchezo, kutokana na walinzi wake kuwadhibiti vizuri washambuliaji wa APR.
Said Bahanunzi aliipatia Young Africans bao la pili katika dakika ya 66, akitumia nfasi hiyo kufuatia makosa yaliyofanywa na mlinzi wa APR aliyetaka kumpiga chenga Bahanunzi kabla ya mlinzi huyo kudondoka ba mpira kumkuta mfungaji akliyeukwamisha bila ajiz nakumuacha mlinda mlango Jean Claud Ndoli akiruka tena bila mafanikio.
Young ASfricans ilifanya mabadiliko ya kuwatoa Said Bahanunzi na Haruna Niyonzima na nafasi zao kuchukuliwa na Jeryson Tegete na Rashid Gumbo, mabailiko ambayo yaliendelea kuisaidia klabu ya Young Africans, kwani iliweza kuwadhibiti vizuri washambuliaji wa APR pamoja na sehemu ya kiungo
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika Young Africans iliibuka na ushindi wa mabao 2- 0hidi wa wageni APR kutoka Rwanda na kukata tiketi ya kucheza robo fainali siku ya jumatatu dhidi ya mshindi wa pili kutoka B.
Young Africans iliwakilishwa na:
1.Berko, 2.Juma Abdul, 3.Oscar, 4.Cannavaro, 5.Yondan, 6.Chuji, 7.Nizar Khalfan/Juma Seif Kijiko, 8.Haruna Niyonzima/Rashid Gumbo, 9.Said Bahanunzi/Jeryson Tegete, 10.Hamis Kiiza, 11.Mwasika
APR : Jean Claude Ndoli, Mbuyu Twite, Kabange Twite, Mugiraneza Jean, Leonel St Preus, Johnson Bagoole, Iranzi Jean Claude, Ngabo Albert, Tuyizere Donatien, Suleiman Ndikumana na Olivier Karekezi.
YoungAfricans News
No comments:
Post a Comment