Wednesday, July 25, 2012

Karekezi: Kagame ikiisha nabaki Yanga


VIONGOZI wa klabu ya Yanga, hivi karibuni waliivamia kambi ya klabu ya APR kwa ajili ya kufanya mazungumzo na nahodha wa timu hiyo, Olivier Karekezi.

Mchezaji huyo anawaniwa vikali na klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Jangwani na Twiga jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Championi Jumatano, Karekezi alisema Yanga imeonyesha nia kubwa ya kumsajili baada ya hivi karibuni kumfuata kambini kwao na kufanya naye mazungumzo.

Karekezi alisema yupo tayari kuichezea klabu hiyo lakini amewatahadharisha viongozi wa timu hiyo wamuache kwanza hadi michuano ya Kombe la Kagame itakapomalizika.

“Najua Yanga wananihitaji kwa ajili ya kuichezea timu yao, lakini nawaomba wasubiri hadi Kagame itakapomalizika, akili yangu hivi sasa inafikiria Kagame tu na siwezi kuchanganya vitu viwili kwa wakati mmoja.

“Kiongozi mmoja wa timu hiyo hivi karibuni alinifuata kambini nikazungumza naye lakini nikamwambia wasubiri Kagame imalizike.

“Nitajiunga na timu hiyo mara baada ya kumalizika kwa Kagame, lakini ifahamike hilo litawezekana tu kama mazungumzo yatakwenda vizuri,” alisema Karekezi.

Na Wilbert Molandi, GPL

No comments:

Post a Comment