Thursday, June 21, 2012

Waliowekewa pingamizi Yanga wapeta


KAMATI ya uchaguzi ya Yanga imeondoa pingamizi dhidi ya wagombea wanne wanaowania nafasi za uongozi katika uchaguzi wa klabu hiyo uliopangwa kufanyika Julai 15.

Wagombe waliowekewa pingamizi ni pamoja na mfanyabiashara maarufu wa jijini Dar es Salaam, kiungo wa zamani wa Yanga Ally Mayayi, Ntanley Kevela na Clement Sanga.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya Yanga kililiambia Mwananchi jana jioni kuwa, pingamizi hizo zimeondolewa baada ya waliolalamika kushindwa kuwasilisha vielelezo vya kuthibitisha madai yako kama walivyotakiwa kufanya.

"Kimsingi kamati ya uchaguzi ilikutana hoteli ya Protea kusikiliza pingamizi dhidi ya wagombea wanne, hata hivyo waliopinga hawakutokea na hakuna pingamizi lililokubaliwa."Kwa maana nyingine, tunaendelea na mchakato mwingine wa uchaguzi keshokutwa, ambao ni usaili," alisema mpashaji huyo.

Awali, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, John Mkwawa aliwataka wanachama waliowasilisha pingamizi kuwasilisha vielelezo vya kuthibitisha madai yao kuanzia saa 4 asubuhi jana ili viweze kufanyiwa kazi na uamuzi kutolewa.
Wanachama wa klabu hiyo waliowasilisha pingamizi kwa wenzao hao ni pamoja na Awadh Juma mwenye kadi namba 07933 na Alfonce John mwenye kati namba 008223 waliomwekea mfanyabiashara huyo maarufu anayewania nafasi ya uenyekiti

Mwingine ni Shamsi Rashid mwenye kadi namba 00374 ambaye alimwekea Yono Kevella anayewania makamu mwenyekiti, Ibrahim Kibede mwenye kadi namba 003353 aliyemwekea Ally Mayayi na Abdalah Mohamed mwenye kadi namba 001702 aliyemwekea Clement Sanga anayewania nafasi ya ujumbe.

Sosthenes Nyoni, Mwananchi

No comments:

Post a Comment