Friday, June 22, 2012

WAGOMBEA UONGOZI WAFANYIWA USAILI


Wagombea nafasi za Uongozi katika klabu ya Yanga leo wamejieleza mbele ya Kamati ya Uchaguzi ya klabu ya Yanga inayoongozwa na Jaji wa Afrika Mashariki Jaji John Mkwawa usaili unaofanyika Ukumbi wa Makao Makuu ya Yanga.
Akizungumza na www.youngafricans.co.tz Mwenyekiti wa Kamati hiyo Jaji Mkwawa amesema wagombea Uongozi watahojiwa kulingana na Kamati ilivyojipanga.
Jaji Mkwawa amesema nafasi zitakazofanyiwa usahili ni pamoja na nafasi nne za wagombea Uenyekiti ambao ni Yusuf Manji,John Nyambele,Sara Ramadhan na Edgar Chibura.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Clement Sanga,Ayub Nyenzi na Stanley Kavela Yono huku mgombea wa nafasi hiyo Ally Mayayi Tembele akiwa ameenguliwa katika nafasi hiyo kutokana na kushindwa kufika katika kamati ya uchaguzi kwa ajili ya pingamizi alilokuwa amewekewa na mmoja wa wanachama.
Katika nafasi ya ujumbe jumla ya wanachama 19 wamejitokeza kuwania nafasi nne za ujumbe.

Source: YoungAfricanFC

No comments:

Post a Comment