Saturday, June 23, 2012

STAA WA BONGO MOVIE ATOA SINGO ‘KUMDISS’ NEY


Nyota kutoka tasnia ya filamu Bongo, Latifah Idabu ‘Badra’ ametoa ‘singo’ inayomchana ‘live’ staa wa Bongo Fleva, Ney wa mitego (mbavu nene).

Akizungumza na Teentz.com muda mfupi uliopita Badra amefunguka kuwa ameamua kutengeneza ngoma hiyo kufuatia kauli chafu dhidi ya wasanii wa kike aliyotowa Ney kwenye wimbo wake mpya wa hip hop ujulikanao kama ‘Nasema nao’ unaotamba hivi sasa kwenye vituo mbalimbali vya redio.

“Nimechukizwa mno na kitendo cha Ney kuimba kuwa mastaa wa Bongo move ni makahaba , hawezi kusema hivyo na sisi tukaa kimya, ametushushia hadhi hasa ukizingatia sisi ni kioo cha jamii, ni zamu yake sasa kusikia nilichomwambia na kama kitamuuma atajibu” alisema Badra na kumalizia kwa t***i.

By Dismas Ten..Teentz

No comments:

Post a Comment