Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jana jijini Dar es Salaam.
***
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga, amewapongeza wachezaji wa Taifa Stars kwa kiwango walichoonyesha kwenye mchezo dhidi ya Gambia, lakini akasema wachezaji wote wa timu hiyo watakatiwa bima ya afya.
Tenga, akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, alisema wachezaji hao walionyesha kiwango cha kuridhisha kwenye mchezo huo, lakini akatupa sifa zake zote kwa kocha Kim Poulsen.
“Nimefurahishwa sana na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wa Stars kwenye mchezo dhidi ya Gambia, hakika kocha amefanya kazi nzuri sana kwa kipindi kifupi alichokaa na timu.
“Wachezaji kama John Bocco na Abubakar Salum walionyesha kiwango kizuri sana, nafikiri timu hii inahitaji sapoti yetu, lakini tumekaa na kukubaliana kuwa wachezaji wote wa timu ya taifa watakatiwa bima ya matibabu.
“Naamini hii itakuwa faraja kubwa kwao, nitafanya kosa kama nitashukuru bila kuishukuru timu ya Azam kwa kutupa mtaalam wao wa mazoezi ya viungo (Paul Gomes), alifanya kazi kubwa sana kwenye timu yetu,” alisema Tenga.
Mbali na hilo, rais huyo aliwaomba mashabiki kuiuga mkono timu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars, inayocheza Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Taifa dhidi ya Ethiopia, Lucy. Katika mchezo wa kwanza wa kutafuta nafasi ya kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika, Twiga ilichapwa mabao 2-1.
Na Khadija Mngwai
No comments:
Post a Comment