Idadi ya waliopoteza maisha kutokana na bomu lililolipuka kwenye baa moja Mombasa Kenya imefikia watatu kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu ambapo wawili walifariki dunia wakiwa hospitali.
Mlupuko huo umetokea Jericho Beer Garden umbali wa kilomita saba kutoka kwenye mji wa Mombasa siku moja tu baada ya ubalozi wa Marekani Kenya kuonya kutokea kwa mlipuko huo, Standard Media Kenya wameripoti kwamba wengi wa watu hao walikua wanatazama mechi ya England na Italy.
Msemaji wa polisi amesema mlipuko ulitokea kwenye mida ya saa nne usiku wa kuamkia leo ambapo wengi wa waliojeruhiwa walikua nje ya baa hiyo huku shuhuda wa tukio hilo akisema mmoja wa waliofariki alikua kwenye dancing floor.
Inaaminika shambulio hilo linaweza kuwa limefanywa na kikundi cha wanamgambo cha Al Shabaab cha Somalia toka Kenya ilipotangaza nacho vita october mwaka jana.
SOURCE: MILLARDAYO BLOG
No comments:
Post a Comment