Monday, June 25, 2012

KITAMBI NOMA WAFUNIKA BONANZA LA TBL, ARUSHA

...yani sssaaaana
kazi ni kazi....akayaaaaah
ubabaifu....
Ze Nomasssss a.k.a Wazee wa NJAA

Klabu inayozidi kuwa gumzo jijini Arusha na Tanzania kwa ujumla...KITAMBI NOMA CLUB jana imedhihirisha kuwa wao ni ZE NOMAS kwelikweli baada ya kufunika bonanza la kila mwisho wa mwezi la kampuni ya bia ya TBL kupitia kinywaji chake cha Grand Malt ambalo hifanyika katika viunga vya General Tyre, Arusha.

Kitambi Noma ambayo iliwekewa zengwe kushiriki katika michuano ya soka ya bonanza hilo ilitia timu viwanjani hapo kuwapa sapoti jirani zao wa damu GEO SECURITY, walioibuka washindi wa bonanza hilo baada ya kuwachalaza 2 - 1 klabu kongwe ya Arusha Wazee. Ze Nomas walifika uwanjani hapo wakitokea kwenye mechi katika uwanja wao wa KIITEC na baada ya kuwachalaza vibayavibaya Access Club kwa jumla ya mabao 7 - 1, na kuendeleza ubabe kwa vibonde hao wa Access Club.

KN (The Nomas) wameendelea kuwa mwiba mkali kwa klabu kongwe za jijini Arusha ikiwemo Arusha Wazee Club kiasi cha wazee hao kuvimba na kununa kwa wivu wa mafanikio ya The Nomas (KITAMBI NOMA CLUB). Kitambi Noma walikuwa wameng'ara na fulanaz zao kali ambalo zilifunika uwanja mzima na kuonekana kama wao ndio waandaaji wa bonanza hilo.

(KWA MAHITAJI YA FULANAZ ZA KITAMBI NOMA WAWEZA FIKA KLABUNI KWAO NA KUJIPATIA KWA BEI NAFUU YA SH. 15,000/= TUH! AU WAWEZA KUWASILIANA NAO KWA NAMBA: 0713-999099 / 0715-414243)

No comments:

Post a Comment