Monday, May 21, 2012

ZE NOMAS (KITAMBI NOMA) ILIVYOIBANJUA ARUSHA ALL STARS 2 - 1 @ GENERAL TYRE GROUND - ARUSHA

Benchi la ufundi la Kitambo Noma
Maelekezo machache kabla ya mechi
Kamati ya ufundi ilisimamiwa vizuri kabisa na Madinda
Erique Mgema 'Chicharito'
Timu zikiwa tayari kwa pambano
Kiungo machachari Ayoub Juma (kushoto) na golikipa Ally Msungi
Nahodha Daud Killo...akimtambulisha mgeni rasmi kwa kikosi chake cha Ze Nomas
Mfungaji wa goli la pili la Kitambi Noma, Sadala
Kikosi kazi cha Kitambi Noma a.k.a Ze Nomas
mtanange ukiendelea


Mapumziko
John Madinda akitoa mawaidha kwa wachezaji wake.

*****
SIKU YA JUMAMOSI (19/05/2012) KATIKA VIWANJA VYA GENERAL TYRE ARUSHA KULIKUWAPO NA BONANZA LA MALIASILI NA UTALII AMBAPO KULIKUWAPO MICHEZO MBALIMBALI IKIWEMO MPIRA WA MIGUU (KABUMBU) HUKU ARUSHA ALL STARS NA KITAMBI NOMA WALIKUWA MOJA KATI YA TIMU ZILIZOALIKWA KATIKA BONANZA HILO, LILILOFANA SANA NA KULETA GUMZO JIJINI ARUSHA.

HUKU KUKITAWALIWA NA MBWEMBWE ZA KILA AINA NA BURUDANI ZA HAPA NA PALE ILIFIKA TAIMU YA KUJUA NANI MBABE KATI YA KITAMBI NOMA (Ze Nomas) NA ARUSHA ALL STARS PANAPO UWANJA ...AMBAPO KATIKA MTANANGE HUO KITAMBI NOMA WALIWABANJUA WATANI WAO WA JADI ARUSHA STARS KWA MABAO MAWILI KWA MOJA (2 - 1). MAGOLI KWA UPANDE WA KITAMBI NOMA YALIFUNGWA NA GODFREI MASANJA NA SADALA HUKU BAO LA KUFUTIA MACHOZI LA ARUSHA ALL STARS LIKIFUNGWA NA Mh. MBUNGE WA JIMBO ARUMERU MASHARIKI, JOSHUA NASSARI.

MCHEZO HUO ULIOSHUHUDIWA NA MAELFU YA WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA ULIKUWA MVUTO WA KIPEKEE KWANI TIMU ZOTE ZILIONESHA UFUNDI KATIKA KUSUKUMA GOZI, LAKINI MPAKA MWISHO WA MCHEZO MZIGO ULIENDELEA KUELEMEA UPANDE WA ARUSHA ALL STARS WAKIONDOKA NA KILIO KINGINE HUKU WAKIMSHUKURU MSHAMBULIAJI WAO TEGEMEZI Mh. JOSHUA NASSARI (MB) KUWAFUTA MACHOZI.

No comments:

Post a Comment