Wednesday, April 4, 2012

Kikao cha kujadili rufaa ya Yanga chavunjika usiku mnene

KAMATI ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo awali ilitoa adhabu kwa wachezaji wa Yanga, jana ilikuwa na kikao cha pamoja na Kamati ya Nidhamu na viongozi wa Yanga, lakini kikao hicho kilivurugika na kuahirishwa.

Kikoa cha kamati hizo kilikuwa ni cha kupitia rufaa iliyokatwa na Yanga baada ya wachezaji wake, Stephano Mwasyika kufungiwa mwaka mmoja, Jerry Tegete miezi sita, Omega Seme na Nurdin Bakari mechi tatu, huku Nadir Haroub Canavaro akifungiwa michezo sita, baada ya wote kutuhumiwa kumpiga mwamuzi Israel Nkongo kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Azam, Machi 10, mwaka huu.

Katika kikao hicho cha kupitia rufaa ambayo ilikatwa na Yanga, chini ya Kamati ya Nidhamu inayoongozwa na Alfred Tibaigana, kilichokaa jana usiku, viongozi wa kamati hizo walianza kuzozana huku kila kamati ikiona kuwa ndiyo ipo sahihi kutoa adhabu.
Kuona hivyo, viongozi wa Kamati ya Ligi ambayo ipo chini ya Wallace Karia ambaye ndiye mwenyekiti, walitoka kwenye kikao hicho na kuondoka.

Hata hivyo, kuliibuka hali ya kutoelewa na viongozi wa Kamati ya rufaa kukumbuka kuwa viongozi wa TFF walitakiwa kuwepo kwenye kikao hicho, lakini walipowaita waliwaambia kuwa hawana nafasi na hivyo kikaahirishwa hadi leo saa kumi jioni.

“Kulitokea hali ya kutoelewa baada ya mabishano huku kila mmoja akimtuhumu nwenzake kuwa hana haki ya kutoa adhabu kwa wale wachezaji wa Yanga. Hali ile iliwakasirisha viongozi wa kamati ya ligi na hivyo walitoka nje na kuondoka ikiwa ni majira ya saa mbili usiku,” kilisema chanzo chetu.

GPL

No comments:

Post a Comment