MNENGUAJI wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, Suzan Chubwa ‘Queen Suzy’, anadaiwa kuvua pete aliyovishwa na mchumba wake, Aimerchard Mwamba ‘G-Seven’. Rafiki wa karibu wa mnenguaji huyo aliyeomba hifadhi ya jina, juzikati alilitonya gazeti hili kuwa, Queen Suzy alichukua uamuzi huo hivi karibuni bila kuweka mezani sababu ya kufanya hivyo. “Habari ndiyo hiyo, hata ukimtafuta sasa hivi na kumwangalia kwenye kidole cha pete utathibitisha hilo. Mimi sijui ni kwa nini kafanya hivyo,” alisema rafiki huyo. Baada ya kupata habari hiyo, mwandishi wetu alimtafuta staa huyo na alipopatikana alitoa maelezo ya kujikanyaga akisema: “Pete ninayo ila huwa navaa pete nyingine kubwa katika kidole hicho. Ile ya uchumba ilikatika, hii wiki ya pili na nimeipeleka kwa sonara sijaenda kuichukua.”
Na Shakoor Jongo, GPL
Na Shakoor Jongo, GPL
No comments:
Post a Comment