SEXY girl, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunua kinywa juu ya skendo zake ambazo ni funga kazi kwa mwaka 2011, The Udaku Master, Ijumaa limembana kwa saa moja na kumpa aya kadhaa ili afunguke, shuka nazo.
KWANZA TUJIKUMBUSHE SKENDO FUNGA KAZI ZA LULU
Miongoni mwa skendo za Lulu zilizotikisa mwaka huu ni pamoja na ile ya usagaji, masuala ya utoaji mimba na kutoka kimapenzi na mapedeshee na waume za watu.
Nyingine ni matumizi ya kinga au kondomu wakati wa tendo la ndoa, kuwa mcharuko na kubwia ulabu kama hana akili nzuri hadi kuzimika kwa nyakati tofauti kwenye klabu za starehe za usiku na hadharani huku suala la kutembea au kukaa nusu utupu nalo likitajwa kumponza.
Katika mfululizo wa skendo hizo, pia Lulu aliwahi kudaiwa kuonesha utovu wa nidhamu kwa mzazi wake (mama) kwa kumtoroka na kwenda kujirusha bila kujali kuwa yeye ni kioo cha jamii na nyuma yake kuna rundo la wasichana wadogo wanaomuiga.
Akizungumza na mapaparazi wa Ijumaa ndani ya ofisi ya gazeti hili, Bamaga-Mwenge, Dar es Salaam, Jumatano wiki hii, Lulu ambaye ni muigizaji bei mbaya kwa sasa Bongo, alichambua skendo hizo moja baada ya nyingine hadi akatokwa na kijasho chembamba.
USAGAJI
Lulu mwenye miaka 18 aliwahi kudaiwa kuwekwa kinyumba na mwanamke mwenzake aliyetajwa kwa jina la Waukweli akihusishwa na masuala ya usagaji.
Kuhusu tabia hiyo mbaya isiyovumilika, alisema: “Nilifahamiana na Waukweli kwa sababu ya mdogo wake tuliyekuwa tunasoma wote. Nilishangaa kusikia naishi na msagaji eti kisa Waukweli ambaye alikuwa na skendo hiyo alikuwa karibu na mimi. Naomba jamii ijue ukweli kwamba sijawahi na sitajaribu uchafu huo.”
UTOAJI MIMBA OVYO
Kuna madai kuwa baadhi ya mastaa wa kike Bongo, Lulu akiwa miongoni mwao, ni hodari wa kuchoropoa mimba ovyo.
Kwa upande wa staa huyo alifafanua: “Mnapo-dili na mastaa wenye tabia hiyo, naomba jina langu lisitajwe hata siku moja kwa sababu sijawahi kubeba ujauzito na sina mpango huo kwa sasa kwani nahitaji kutengeneza maisha ili hata siku nikipata mtoto awe na maisha bora.”
KUTOKA KIMAPENZI NA MAPEDESHEE
Lulu aliwahi kukumbwa na skendo ya kuhongwa nyumba na mbunge mwenye kitambi kutoka mikoa ya Kusini mwa Tanzania (jina tunalo) na baadaye ilidaiwa kuwa ukarabati wa nyumba hiyo ulifanywa na pedeshee maarufu jijini Dar (naye jina tunalo).
Kuhusu hilo, msanii huyo hot alifunguka:
“Baada ya stori ile kujaa tele kwenye gazeti lenu la Ijumaa Wikienda, mheshimiwa (huku akimtaja jina) alinipigia simu na kuniuliza juu ya suala hilo. Nilishtuka sana kwani nafahamiana naye tu ila nyumba nilijenga mwenyewe. Nilimweleza ukweli na nikamwambia mimi sijui chochote.
“Jamani! Jamani! Naomba mashabiki wangu wanielewe, sijawahi ‘kutoka’ na pedeshee yeyote pamoja na kwamba wananitongoza kila kukicha, tena wengine ni watu ninaowaheshimu sana. Siwezi kufanya kitu ka’ hicho.”
VIPI LULU ANATUMIA KINGA KWENYE TENDO LA NDOA?
Kwenye makabrasha ya Ijumaa kuna listi ya mastaa wa kike waliowahi kukiri kutotumia kondomu wakati wa tendo la ndoa bila kujali gonjwa la Ukimwi na matokeo yake waliambulia mimba wasizotarajia, kuhusu hilo, Lulu alisema:
“Nawaonea huruma sana. Haiwezi kutokea kwangu, hakuna kitu ambacho huwa niko makini nacho kama hicho kwani najali afya yangu.”
LULU MCHARUKO
Staa huyo mwenye jina kubwa ndani na nje ya Bongo kupitia filamu na video za wasanii wa Bongo Fleva, aliwahi kutamba kuwa miongoni mwa mastaa wa kike nchini yeye ni mcharuko namba moja.
Katika hilo aliweka mambo sawa: “Kwa sasa nimebadilika sana, mimi siyo yule Lulu wa zamani. Kwanza nimekua na ndiyo maana sitaki kuitwa Lulu tena, natamani niitwe Lizzy ili kuonesha kuwa mimi siyo mcharuko tena.”
UCHAPOMBE
Mara kadhaa Lulu aliwahi kuripotiwa kulewa tilalila na kufanya mambo ya aibu (hayafai kufafanuliwa kwa watoto chini ya miaka 18), alipopewa nafasi na Ijumaa kufafanua juu ya hilo, alisema:
“Nilishawaomba Watanzania wanisamehe katika hilo na nazidi kuwaahidi kuwa hali hiyo haitajirudia kwani ule ulikuwa utoto tu.”
WAUME ZA WATU
Msanii huyo kinda aliwahi kukumbwa na skendo ya kupora mume wa mtu na adhabu yake ilikuwa ni kuchanwa viwembe usoni na mwanamke ‘mwenye mali’ hivyo kumharibu vibaya sehemu ya paji la uso wake.
Akifafanua juu ya skendo hiyo, Lulu alifunguka: “(huku akipapasa kovu la viwembe usoni) sina tabia hiyo. Kilichotokea ni kwamba yule mwanamke alihisi natembea na mumewe, lakini ukweli ni kwamba jamaa alikuwa ni rafiki yangu wa kawaida tu na hata mkewe huyo alikuwa anajua kwa hiyo si kweli kwamba mimi ni hodari wa waume za watu.”
KUTEMBEA/KUKAA UCHI
Kwa kumuona tu, huwezi kuuliza kama Lulu anapenda kutembea au kukaa uchi kutokana na mavazi yake. Vilevile aliwahi kuponyokwa na maneno kinywani mwake kuwa akivaa nguo ndefu huwa anawashwa.
Katika hilo, alisema: “Napenda sana miguu yangu kwani ni mizuri ndiyo maana huwa naiacha wazi. Si kweli kwamba napenda kukaa uchi. Kuna watu wangapi mitaani wanatembea utupu lakini hawaonekani? Najua ni kwa sababu mimi ni staa ndiyo maana ni rahisi kwa watu kusema.”
MPENZI WAKE NI NANI?
Lulu: “Kwa sasa sina mpenzi. Nilikuwa naye lakini tumeachana kwa kuwa nahitaji kuwa peke yangu.”
ANATAKA KUOLEWA NA MWANAUME GANI?
Alisema: “Mwanaume yeyote atakayenipenda kwa dhati, awe staa, asiwe staa, tajiri au maskini.”
NENO LA IJUMAA
Kwetu sisi Lulu ni miongoni mwa vijana watafutaji wanaopaswa kuigwa. Ameahidi kwa kinywa chake kuwa amebadilika hivyo ni matumaini yetu kuwa atatunza maneno aliyoyatamka ili kujiwekea hazina ya heshima mbele ya jamii.
Na Brighton Masalu na Imelda Mtema, GlobalPublishersTz

No comments:
Post a Comment