Friday, November 25, 2011

GPL: SuperSport kurusha Chalenji Kiswahili


MICHUANO ya Kombe la Chalenji inayoanza leo jijini Dar es Salaam, itaonyeshwa moja kwa moja na kituo cha SuperSport cha Afrika Kusini.

Mbali ya kituo hicho cha televisheni kurusha moja kwa moja michuano hiyo inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), habari nzuri zaidi ni kwamba, maoni ‘comments ‘ za mchezo zitakuwa zikitolewa katika lugha ya adhimu ya Kiswahili.

Ofisa Uhusiano wa MultChoice Tanzania, Barbara Kambogi, amesema wahusika katika mchakato huo wa kutoa maoni ni Ali Salim Mmanga, Jack Oyoo Sylvester, Ali Hassan Kauleni, Japheth Kahindi Charo, Florian Kaijage aliyekuwa ofisa habari wa TFF na Clifford Ndimbo aliyekuwa msemaji wa klabu ya Simba.

Aidha, taarifa ya Gary Rathbone, ambaye ni Mkuu wa Operesheni ya Supersport barani Afrika, imesema: “Soka ni mchezo wa watu, ndiyo maana SuperSport imekuwa ikifanya iwezavyo kuwafikia watu.

“Kituo chetu kupitia DStv kinawapa nafasi mashabiki wa soka wa Afrika Mashariki kuburudika zaidi kwa kuwatangazia katika lugha ya Kiswahili ambayo inatumiwa na watu wengi wa ukanda huo.” 

No comments:

Post a Comment