Monday, September 19, 2011

Taasisi ya THT yaadhimisha mahafali ya sita jijini dar.

Pichani ni baadhi ya wasanii waliopitia kwenye kituo hicho cha THT,na kuonesha mafanikio kwa kiasi kikubwa katika anga ya muziki hapa nchini.Kulia ni Msanii Mwasiti.LIna.Ditto pamoja na Amin wakiimba kwa pamoja katika mahafali hayo,yaliyofana kwa kiasi kikubwa.

Wasanii hao wapatao 30 wakiimba mbele ya wageni waalikwa kuonesha ni kiasi gani wameiva katika fani ya muziki,ingawaje hiyo ni hatua ya kwanza kwa wahitimu hao.


Mwanamuziki Mkongwe na kutoka kundi la The Kilimanjaro Band a.k.a Wananjenje,Waziri Ally akiongea mbele ya wageni waalikwa pamoja wasanii mbalimbali waliolikwa katika mahafali hiyo ya sita,iliofayika jioni ya leo jijini Dar,kushoto kwake ni Mwanamuziki mahiri Dada Carola Kinasha ane akisubiri kutoa maoni yake kuhusiana na mahafali ya watoto hao wapatao 30.

Pichani kati ni mmoja wa walimu wa muziki THT,Cadinal Gento akikata keki jioni ya leo wakati taasisi hiyo ilipokuwa ikifanya mahafali ya sita kwa vijana wake 30 wanaomaliza mafunzo ya muziki,ambapo hafla imefanyika leo maeneo ya Morocco Block 41 nyuma,ya mgahawa wa Bestbite ambako ndiko kwenye tukio husika la THT. Kulia ni mmoja wa wanafunzi wanahotimu,Twaha Khalfan pamoja na mratibu wa hafla hiyo,Teacher Nkya wakishuhudia tukio hilo la ukataji keki.

Habari Picha na Michuzi Jr, JIACHIE BLOG

No comments:

Post a Comment