Wednesday, September 7, 2011

Idd Azzan aonesha njia kumsaidia Mzee Kipara.



Siku chache baada ya Kampuni ya Global Publishers kumsaidia msanii mkongwe wa tasnia ya maigizo na filamu nchini, Fundi Said ‘Mzee Kipara’ (pichani)kupata simu, Mbunge wa Kinondoni jijini Dar es Salaam kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Idd Azzan naye ameguswa na hali ya mzee huyo na kuamua kuonesha njia kwa kutoa msaada wa shilingi laki mbili kwa ajili ya matibabu ya miguu yanayomsumbua galacha huyo.

Azzan ambaye alifunga safari mpaka Kigogo Mbuyuni jijini Dar anakoishi Mzee Kipara, alisema kwa mara ya kwanza alisoma habari ya kuumwa kwa mkongwe huyo kwenye gazeti hili. Anasema aliumia sana moyoni kumuona Mzee Kipara akipata mateso kwa sababu ya kukosa fedha za kutibu tatizo lake la miguu kuishiwa nguvu na kuuma kwa kipindi kirefu, hali inayowasikitisha wengi.

Kwa watu wengine wenye moyo wa upendo na huruma wanaombwa wamsaidie Mzee Kipara ili apate fedha za matibabu na matumizi madogo, watume michango yao kupitia huduma ya M-PESA au Tigo Pesa kwa namba 0753 923 454 ambayo imesajiliwa, michango hiyo itamfikia mlengwa moja kwa moja.


Na Shakoor Jongo, Global Publishers Tz

No comments:

Post a Comment