Tuesday, September 20, 2011

Abdallah Idrisa Majura awa mwandishi wa kwanza Tanzania kumiliki kituo cha redio nchini

Mmiliki wa SPORT FM 91.2 Abdallah Idrisa Majura akiangalia leseni ya umiliki wa kituo chake alichopokea toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya mawasilianao Tanzania (TCRA) Profesa John Nkoma (picha: Michuzi blog).

Abdallah Idrisa Majura, mmiliki wa Sport FM 91.2 amepokea rasmi leseni ya umiliki wa kituo tajwa cha redio kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya mawasilianao Tanzania (TCRA) Profesa John Nkoma.

Majura ambaye amewahi kufanya kazi Radio Tanzania, ITV/Radio One Stereo na BBC ni mtangazaji na mwandishi wa habari wa kwanza nchini Tanzania kumiliki kituo cha Redio, nchini Tanzania.


Habari na Wavuti.Com

No comments:

Post a Comment