Friday, August 5, 2011


Na Ahadi Kakore na Lucy Mgina
KOCHA wa Taifa Stars, Jan Poulsen hatamwita kiungo mshambuliaji wa Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ hadi atakapojirekebisha kutokana na kile alichoeleza kuonyesha utovu wa nidhamu.

Poulsen amesema hayo kufuatia Boban kutojiunga katika kikosi cha vijana chini ya miaka 23, Manyara Stars, kilichocheza mechi ya kirafiki mkoani Arusha hivi karibuni dhidi ya Shelisheli, ili kuona uwezo wake kabla ya kumjumuisha kwenye kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars.

“Boban alionyesha utovu wa nidhamu na akashindwa kwenda na kikosi bila kutoa taarifa zozote, kwa maana hiyo ninaweza kumuita ikiwa ataomba radhi kwa alichokifanya, kwani licha ya kuwa na kiwango kizuri lakini siwezi kuwa na mchezaji ambaye hana nidhamu,” alisema Poulsen.

Kutokana na kushindwa kujiunga katika kikosi cha Manyara Stars, Boban alielekea Zanzibar ambapo klabu yake ya Simba ilikuwa imekweka kambi, ikijiandaa na msimu mpya wa ligi.

No comments:

Post a Comment