Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mkoa wa Mara, Ester Bulaya.
Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee.
Kama ni uongo, basi huu utakuwa umepitiliza na ikiwa tuhuma hizi ni za kweli, itakuwa ni aibu kwa sababu madai yanayozagaa mjengoni ni kwamba, Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee ana uhusiano wa kimapenzi na mwenzake wa Viti Maalum (CCM), Mkoa wa Mara, Ester Bulaya.
Tuhuma hizo zinadai kuwa, Halima na Ester wana uhusiano wa vitendo vya usagaji kwa muda mrefu, huku wakigeuka gumzo ndani na nje ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
NI GUMZO BUNGENI
Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde alisema kuwa tuhuma hizo za Halima na Ester kuwa na uhusiano usiofaa ameshazisikia lakini hana uhakika nazo.
“Ni habari ambazo tunazo lakini sina uthibitisho. Huo ndiyo ukweli wangu.”
Wabunge wengine waliozungumza na gazeti hili, kila mmoja alikiri kusikia tuhuma za wabunge wawili wanawake kuwa na uhusiano wa kisagaji lakini waligwaya kutaja majina ya wahusika.
IDD AZZAN, KINONDONI (CCM)
“Hizo tetesi nimeshazisikia lakini sijui kwa undani. Hayo mambo yanasemwa bungeni lakini siwezi kuwataja kwa majina kwa sababu hakuna aliyewahi kuthibitisha.”
DAVID KAFULILA, KIGOMA KUSINI (NCCR-MAGEUZI)
“Kuna tetesi za namna hiyo, ingawa mazingira ya siasa za Tanzania usiwe mwepesi kuamini katika tetesi, ndiyo maana mimi kama kiongozi siwezi kuzungumzia tetesi na vitu ambavyo sina uhakika navyo.”
AESHI HILALI, SUMBAWANGA MJINI (CCM)
“Nimeshasikia watu wanazungumza lakini sina uhakika. Siwezi kuwataja majina kwa sababu sijawahi kuthibitisha, ingawa ni ukweli kwamba hilo linazungumzwa karibu bunge zima.”
FELIX MKOSAMALI, MHAMBO (NCCR-MAGEUZI)
“Ha ha haa, nimewahi kusikia hizo habari lakini hawajawahi kufumaniwa, kwa hiyo hakuna mwenye uhakika. Mimi siwezi kuwa shahidi kwa sababu sijawahi kushuhudia chochote zaidi ya kusikia habari za watu.”
Hata hivyo, kuna wabunge walikanusha.
JOSEPH MBILINYI ‘SUGU’, MBEYA MJINI (CHADEMA)
“Dah, hizo habari kwangu ni mpya. Sijui kabisa.”
REGIA MTEMA, VITI MAALUM (CHADEMA)
“Hizo tuhuma za watu kuwa na uhusiano wa kusagana sijawahi kuzisikia popote.”
SPIKA MAKINDA NAYE?
Spika wa Bunge, Anne Makinda alipopigiwa simu ili atoe ufafanuzi wa jambo hilo, alisema kuwa hawezi kuzungumza kwa sababu yupo safarini. Hata hivyo, hakusema anakotoka na wala anakoelekea.
Ijumaa Wikienda lisingeweza kwenda kiwandani bila kuwapa nafasi ya msingi watuhumiwa hao kujieleza kuhusu madai hayo.
Kwa upande wake, Halima alikiri kuwepo kwa shutuma hizo ambapo alisema si ngeni na kwamba ilianza kuchanua kipindi cha Uchaguzi Mkuu 2010, kwani wapinzani wake walitaka kuitumia kama silaha ya kumshinda, hata kwenye magazeti ilichapishwa.
“Kwanza nashukuru sana kwa kunipa nafasi hii ya kujieleza, si madai mapya, ni ya siku nyingi sana. Yalianza wakati wa Uchaguzi Mkuu 2010, baadhi ya magazeti yakaandika. Aisee, ni siasa tu hizi,” alisema Mdee.
Akaongeza: “Mimi ni public figure (mtu wa jamii) kwa hiyo kusemwa au kusingiziwa ni vitu vya kawaida, maadui wapo na marafiki pia.
“Hata hivyo, naangalia maisha yangu, siwezi kuishi kwa hofu ya nani atasema nini. Hayo mambo ni ya kisiasa lakini hayana ukweli. Wanaonifahamu, wanajua naishi vipi, toka sekondari hadi chuo kikuu.
“Lakini ndugu (mwandishi) nasisitiza, madai hayo si ya kweli, hakuna kitu kama hicho kwangu.”
Kwa upande wa Bulaya, alipopigiwa simu, Julai 23, mwaka huu saa 9: 52, 9:59, 10:28, mara zote iliita na kukatwa.
Na Global Publishers Tz
No comments:
Post a Comment