Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akiwaongoza viongozi wa Kiserikali wakati wa heshima maalum kwa ajili ya kuwaombea Mashujaa waliopigana vita katika aridhi ya nchi ya Msumbiji, ambapo jumla ya miili ya askari 101 walihamishwa kutoka Msumbiji mwaka 2004 na kuzikwa katika Makaburi Naliendele mkoani Mtwara kati ya 108 waliofariki katika vita hivyo. Sherehe hizo za kuwakumbuka mashujaa hao zimefanyika leo Julai 25, 2011 katika viwanja vya makaburi hayo mkoani Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akiweka Mkuki, katika Mnara wa Mashujaa mahala walipozikwa Mashujaa 101 waliopigana vita Msumbiji, ikiwa ni siku ya sherehe ya kuwakumbuka Mashujaa iliyofanyika kwenye Viwanja hivyo vilivyopo Naliendele mkoani Mtwara leo Julai 25, 2011.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete na Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakitembelea kukagua makaburi 101 kati ya 108, ya askari ‘Mashujaa’ walifariki wakati wakipigana vita Msumbiji na kuzikwa katika Makaburi ya Naliendele mkoani Mtwara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Wazee waliopigava Vita, ambao ni sehemu ya mashujaa wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment