Mtangazaji mahiri wa Clouds FM,Ruben Ndege a.k.a Ncha Kali akifanya mahojiano mafupi na Mwanamuziki Ludacris mapema leo.
Ludacris akiacha chata lake mjengoni.
Mwanamuziki Ludacris akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa Clouds Media Group leo mchana,kwenye ofisi za kampuni hiyo,Mikocheni jijini Dar.
Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba,kati ni Mwanamuziki/Muigizaji Ludacris kutoka Marekani na Allan Chonjo,Meneja wa Bia ya Serengeti ambao ndio wadhamini wakuu wa
tamasha la Fiesta 2011.
Mkurugenzi wa Utafiti wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akifafanua jambo kwenye mkutano wa Waandishi wa habari mapema leo asubuhi kwenye hoteli ya Kempisnk kuhusiana na onyesho la kesho litakalofanyika kwenye viwanja vya Lidaz Club Kinondoni jijini Dar,litakalomuhusisha Mwanamuziki Ludacris (wa pili kutoka kulia). Kushoto ni Caroline Ndungu, Mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti Breweriers anayemaliza muda wake na Meneja wa bia ya Serengeti Premium Lager Allan Chonjo.
Habari Picha na MICHUZI JR
No comments:
Post a Comment