Monday, January 2, 2012

VODACOM BABATI HALF MARATHON YAFANA MANYARA.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Elaston Mbwilo mwenye truck suit nyeupe akipuliza kipenga kuashilia kuanza kwa Mbio za Vodacom Babati half Marathon kwenye office za Manyara Internet café. Kulia kwake ni Meneja masoko wa Vodacom Kanda ya kaskazini ndugu Jerome Munisi.

Mshindi wa kwanza wa Mbio za Vodacom Babati half marathon kwa upande wa wanaume ndugu Sambu Andrea kutokea club ya Arusha sport Arusha akiingia kwenye viwanja vya Kwaraa mjini Babati. Alitumia muda wa 1:04:51:97.

Mshindi wa kwanza wa Mbio za Vodacom Babati half marathon kwa upande wa Wanawake Bi.Catherine Langa kutokea Arusha akiingia kwenye viwanja vya Kwaraa mjini Babati. Alitumia muda wa 1:20:15:88.

Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Manyara Mh. Elaston Mbwilo akitoa hotuba kwa wananchi pamoja na washiriki wa mashindano ya Vodacom babati half marathon kwenye viwanja vya Kwaraa mjini Babati. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa mashindano hayo ndugu Mohamed Bajwa, Mbunge wa Babati vijijini Mh. Jituson Patel (CCM), Mbunge wa viti maalum Chadema Mh. Paulina Gekuu na Meneja Masoko kanda ya kaskazini ndugu Jerome Munisi.

Washindi wa mbio zote wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi pamoja na wadhamini Vodacom na waheshimiwa wabunge wa mkoa wa Manyara.


Katika kusherehekea sherehe za kuuaga mwaka 2011 mjini Babati Manyara, kulifanyika mashindano ya Vodacom Babati half marathon (KM 21). Mbio hizo zilidhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom. Mgeni rasmi katika mashindano hayo alikuwa ni mkuu wa mkoa Mh.Elaston Mbwilo akiambatana na uongozi mzima wa mkoa wa Manyara yaani mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Babati, Mkuu wa polisi Mkoa, Mbunge wa Viti maalum Chadema Mh. Paulina Gekuu na Mbunge wa CCM Babati vijijini Mh. Jituson Patel.

Habari Picha na Riziki Mwalupindi

No comments:

Post a Comment