Friday, December 30, 2011

BREAKING NEWS: John Ngahyoma wa BBC hatuanye tena


John Ngahyoma(pichani), Mwandishi mkongwe wa habari Tanzania na Mtangazaji amefariki dunia hii leo asubuhi.

Kifo cha Ngahyoma aliyekuwa mtangazaji na mwandishi wa shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) nchini Tanzania akiripoti kutoka Dar es Salaam na viunga vyake kimekuja siku moja baada ya mtangazaji mwingine mkongwe wa kike aliyejizolea sifa kubwa ya utangazaji mpira Haklima Mchuka kufariii ghafla huku mipango ya maziko yake ikiendelea.

Ngahyoma aliyewahi kufanya kazi katika vituo vya taifa vya redio cha Redio Tanzania Dar es Salaam na baade kujiunga na IPP Media katika vituo vya Redio One na ITV ambako pia aliondoka na kujiunga na BBC ameripotiwa kufariki hii leo jijini Dar es Salaam.

Tasnia ya habari nchini Tanzania kwa kipindi cha siku mbili itakuwa imeapatwa na pigo kubwa kufuatia vifo vya waanahabari hao wawili wa siku nyingi.
Marehenu Ngahyoma amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu na hata kwenda nchini India kwa matibabu zaidi kufuatia maradhi yaliyokuwa yakimsibu.

Taarifa ya haraka iliyotumwa katika mitandao ya kijamii (blogs) na Katibu Mkuu wa Jukwaa la wahariri (TEF) Neville Meena inasema msiba upo nyumbani kwa marehemu Tabata Segerea jijini Dar es Salaam jirani na kwa Mwandishi mwingine aliyefariki miezi kadhaa iliyopita Danny Mwakiteleko.

Aidha Meena ameomba mtu yeyote atakaekuwa na taarifa zaidi kuhusiana na mipango ya maazishi ya Marehemu Ngahyoma kumfikishia.

Blog hii inaungana na wanahabari wote Tanzania na duniani kutoa pole kwa familia ya marehemu akiwepo, mke, watoto, ndugu jamaa na marafiki wote kwa msiba huo mkubwa uliowafika wakati huu wa shamra shamra za mwaka mpya.

Mungu awatie nguvu na imani wote waliofikwa na Msiba huu.

Bwana Mungu alitoa na Bwana Mungu ametwaa Jina lake lihimidiwe.

Habari na Faza Kidevu

No comments:

Post a Comment