Friday, November 18, 2011


UHUSIANO wa kimapenzi wa wasanii wa muziki Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’ na Ally Timbulo waliouanzisha na mastaa wa filamu Bongo, Wema Sepetu na Jacqueline Pentzel unadaiwa kuwamaliza kisanii kutokana na kutumia muda mwingi kitandani.

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, mwanamuziki mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake alidai kuwa, tangu madogo hao wajiingize kwenye mapenzi na mademu hao, maisha yao kimuziki yamebadilika na wakati mwingine kuhisi bora mapenzi kuliko kazi.

“Unajua mimi ni rafiki wa karibu wa Diamond na Timbulo, wanakoelekea siko kabisa na ukiwafuatilia sana utabaini mapenzi yanawamaliza, wasipojiangalia wanaweza kuyeyuka kwenye anga la muziki.

“Kuna wakati washikaji wanapigiwa simu za madili, lakini kwa kuwa wako na wapenzi wao maeneo, wanachomolea. Kimsingi wale mademu ni wasanii na wanayajua mapenzi hivyo wanawachanganya sana.

“Mcheki hata Diamond, mauno aliyokuwa akikatika kipindi cha nyuma hatuyaoni kwa sababu muda mwingi anautumia ‘on bed na baby’ wake Wema, Timbulo ndiyo kwanza hasikii la kuambiwa kwa Jack,” alidai mtoa habari huyo.

Baada ya kuikamatia ishu hiyo, paparazi wetu aliwatafuta mastaa hao na hiki ndicho walichokisema kuhusiana na madai hayo:
TIMBULO: Watu wanaweza kusema mengi lakini kiukweli mapenzi yangu na Jack hayaniathiri chochote katika kazi yangu ya muziki. Nina muda wa kuwa na mpenzi wangu na nina muda wa kazi, wanaohisi nimekwisha waje pale Maisha Club Jumapili hii waone shoo yangu.

JACK: Kwa kifupi unapokuja muda wa kufurahia mapenzi yetu, kazi zetu tunaweka pembeni na linapokuja suala la kazi, mapenzi yanakaa pembeni. Sidhani kwamba penzi langu linammaliza kisanii Timbulo.

DIAMOND: Kusema kweli inafikia wakati inanibidi kuwa karibu sana na mpenzi wangu, kwani hata leo hii (Jumatano) jioni nitaondoka kwenda South Africa na baby wangu kwa ajili ya kupumzika.

Mapenzi yapo na muziki upo na naamini Wema haniathiri kimuziki bali ananipa changamoto za kimaisha.
Wema hakupatikana mara moja kuzungumzia ishu hiyo.

Hivi karibuni Timbulo alianzisha uhusiano wa kimapenzi na Jack akifuata nyayo za msanii mwenzake Diamond ambaye amezama kwenye dimbwi la mapenzi na Wema.

Na Musa Mateja

No comments:

Post a Comment