Hot and sexy lady’ kwenye tasnia ya filamu Bongo, ambaye ni mpenzi wa mwanamuziki Naseeb Abdul ‘Diamond’, Wema Sepetu hivi karibuni alinaswa kwenye gesti moja iliyopo Kinondoni, Dar es Salaam akiwa na msanii mwenzake, Yusuf Mlela.
Wawili hao walipigwa chapo na mdaku wetu Septemba 26, mwaka huu mishale ya saa 3 asubuhi katika nyumba hiyo ya kupumzikia na kuburudikia inayofahamika kwa jina la Jokko.
Awali, mtoa habari wetu alilipigia simu gazeti hili akidai kuwaona mastaa hao eneo hilo hivyo kumtaka mwandishi wetu kufika haraka ili awafotoe picha.
“Hapo ni gazeti la Ijumaa eee…? Sasa nyie si mmesema mnanunua habari? Njooni hapa Kinondoni, gesti ya Jokko yupo Wema na Mlela, fanyeni fasta kabla hawajaondoka,” alisema sosi huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Katika kuhakikisha tukio hilo linanaswa live bila chenga, usafiri wa daladala ulionekana kutofaa hivyo paparazi wetu alidandia babaji na kumtaka dereva kumkimbiza kwenye eneo hilo.
Hata hivyo, jitihada za kunasa mastaa hao eneo hilo ziligonga mwamba baada ya kufika na kutonywa kuwa, walikwishaondoka.
“Aaa umechelewa wameondoka sasa hivi wakiwa kwenye gari, muda ule napiga simu ndiyo walikuwa wanatoka hapa, huenda walilala au walikuja asubuhi hii ila nimewaona kwa macho yangu Wema na Mlela,” alidai mtoa habari huyo.
Katika kuzithibitisha habari hizo, mwandishi wetu alimpigia simu Wema, alipopatikana alisema ni kweli alikwenda pale kumfuata Mlela ila ilikuwa ni kwa mazungumzo ya filamu wanayotaka kucheza.
“Ni kweli nilikwenda, Mlela aliniambia yuko pale hivyo nikamfuata kwa ajili ya mazungumzo ya filamu yetu tunayotarajia kuicheza hivi karibuni, kimsingi tulikuwa kikazi na si vinginevyo,” alisema Wema.
Hata hivyo, katika hali iliyoonesha huenda kuna kitu, Mlela alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo alikana huku akieleza kuwa, siku hiyo hakuonana kabisa na Wema.
“Siyo kweli bwana, sikuwa na Wema hiyo jana na wala sikuonana naye kabisa, kama mna picha nyie zitoeni kwanza,” alisema Mlela.
Wakati hayo yote yanatokea, Diamond ambaye ni mpenzi na Wema alikuwa kwenye ziara ya kimuziki nchini Rwanda na Burundi.
Na Global Publishers Tz
No comments:
Post a Comment