Friday, June 3, 2011
Tupande miti ili kuepuka madhara yatokanayo na uharibifu wa mazingira nchini - Dr. Bilal
Akizindua maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani mkoani Ruvuma, juzi, Dk. Bilal alisema upo umuhimu mkubwa wa kutunza rasilimali hizo kwa kuzingatia ongezeko la watu.
Dk. Bilal alisema takwimu zinaonesha takribani hekta zipatazo 400,000 za misitu hupotea kila mwaka wakati asilimia 90 ya nishati inayotumika nchini inatokana na miti. Nishati ya mafuta inayotumika ni asilimia saba.
Alisema vyema wananchi wanapoadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara ambao kilelele chake ni Desemba 9 mwaka huu, miaka 50 ijayo idadi ya watu huenda ikaongezeka na kufikia milioni 100 wakati rasilimali zinazotegemewa zikiwa haziongezeki. “Hivyo ni vyema wakazitunza kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo,” alisisitiza.
Ujumbe wa kimataifa wa maadhimisho hayo mwaka huu ni ‘tumethubutu; tumeweza na tunazidi kusonga mbele’ wakati ujumbe wa kitaifa ni ‘miaka hamsini ya uhuru, panda miti na kuitunza: hifadhi mazingira’.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment