Friday, June 3, 2011

Babu asitisha huduma Jumapili


MCHUNGAJI Ambilikile Masapila ‘Babu’ wa Kijiji cha Samunge, Loliondo mkoani hapa, amesitisha utoaji dawa Jumapili kuanzia sasa kwa lengo la kufanya ibada zaidi ili Mwenyezi Mungu amfunulie uwezo zaidi wa kuponya magonjwa sugu na kupata mapumziko baada kutoa tiba hiyo kwa muda mrefu.

Wakati Babu akitoa angalizo hilo, serikali mkoani hapa imetoa onyo dhidi ya matapeli wanaouza vibali bandia vya kuyaruhusu magari kwenda Samunge kupeleka wagonjwa kupata kikombe cha Babu wakati vibali hivyo hutolewa bure.

Msaidizi wa Babu, Bw. Frederick Nisajile alisema kuwa mchungaji huyo kwa kupata muda zaidi wa kufanya ibada siku hiyo pamoja na mapumziko ya kutosha ni wazi atafanya kazi zake kwa ufanisi zaidi.

Tangu Babu aanze kutoa tiba hiyo iliyowavuta wagonjwa wengi kutoka ndani na nje ya nchi kwa zaidi ya miezi nane sasa, huku akitoa kikombe kwa wagonjwa zaidi 2,000 kwa siku hajawahi mkupata mapunziko ya kutosha kwani hata siku ya Jumapili amekuwa
akiendela na tiba baada ya kutoka kanisani.

“Kama binadamu kufanya kazi nzito kama hiyo kwa muda mrefu bila kupumzika … kwa miezi hiyo anastahili kupumzika na kuwasiliana na Mungu wake kwa utulivu zaidi hasa siku za Jumapili..lakini wagonjwa wasihofu tiba itakuwepo kama kawaida,” alisema.

Akizungumzia idadi ya wagonjwa wanaoingia kijijini hapo, kupitia vituo mbalimbali alisema wanapata kikombe bila bughudha yoyote na kurudi makwao ndani ya siku moja kutokana na kutekelezwa kwa taratibu kadhaa zilizowekwa na serikali.

Ofisa Habari Ofisi ya Mkoa wa Arusha, Bw. Yotham Ndembeka kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Isidore Shirima kuwa imegundulika kuwepo kwa matapeli wanaouza vibali na kuwataka wananchi kujihadhari nao.

Alisema vipo vibali bandia vilivyozagaa Arusha na vinauzwa (hajataja bei) kwa wagonjwa wanaoelekea kwa babu, serikali imelitambua hilo na inalifanyika kazi suala hilo kikamilifu kwani mamlaka husika zimeshaanza kazi.

Kuhusu kusitishwa kwa tiba siku ya Jumapili, alisema kwa wiki serikali itatoa vibali vya kuondoa hadi siku ya Ijumaa ili wagonjwa wapate tiba siku ya Jumamosi na kurudi na hakuna kibali kitakachotoka Jumamosi.

Aliwataka madereva wanaosafirisha wagonjwa kuendesha ma gari yao kwa mwendo wa wastani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika kwani baada ya serikali kufanya ukarabati wa barabara ya kuelekea kijijini Samunge na kuwa nzuri baada ya
ukarabati madereva hao wamekuwa wakienda mwendo wa kasi.


Source: Majira

No comments:

Post a Comment