Friday, June 17, 2011

RPC KILIMANJARO, LUCAS NG'HOBOKO AFARIKI DUNIA


Taarifa kupitia Radio Uhuru na Radio One Stereo zinasema kuwa aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kilimanjaro na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, SACP, kabla ya kustaafu utumishi wa umma, Lucas Ng'hoboko amefariki dunia.

Marehemu Ng'hoboko amefariki leo katika hospitali ya Kilimanjaro Christian Medical Centre, KCMC, wakati akipatiwa matibabu alipowahishwa hapo majira ya asubuhi kwa matibabu zaidi.

Audio iliyorekodiwa na Dullonet.com toka Radio One Stereo ambapo mtangazaji Deo Rweyunga alikuwa akihojiana na Kaimu Kamanda wa mkoa Kilimanjaro, Afisa Mnadhimu Yusuph Ilembo, inathibitisha kutokea kwa kifo hicho.

Ilembo amesema Marehemu Ng'hoboko alipofika kwenye Zahanati ya Polisi majira ya saa tatu asubuhi kwa ajili ya kuchunguzwa afya yake kwa kutokujisikia vizuri, ghafla alianguka na ndipo juhudi za kumwahisha hospitalini KCMC kwa matibabu zaidi zilifanyika. Akasema baada ya muda mfupi, alipigiwa simu kufahamishw akuwa Ng'hoboko amefariki dunia.

Mwili wa Marehemu Ng'hoboko umehifadhiwa katika hospitali ya KCMC kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Taratibu za maziko zinafanywa kwa ushirikiano baina ya familia ya marehemu na Jeshi la Polisi.

Salam za faraja kwenu nyote mlioguswa na msiba huu.

Apumzike pema marehemu Lucas Ng'hoboko.

source: http://www.wavuti.com/4/post/2011/06/rpc-kilimanjaro-lucas-nghoboko-afariki-dunia.html#ixzz1PXyWeVNT

No comments:

Post a Comment