Friday, June 17, 2011

Mtoto auawa kwa udokozi wa Sh. 3,500/=

SIKU moja baada ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Africa, Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia mtu mmoja kwa kosa la mauaji ya kikatili kwa mtoto mdogo kisa wizi wa Sh. 3,500/=

Anayeshikiliwa na jeshi hilo ametajwa kwa jina la Shedi Mdeka(40) mkazi wa eneo la RRM Jijini Mbeya ambapo amemuua Vick Christopher (9) ambaye alikuwa ni mtoto wa mdogo wake.

Kifo hicho kimeelezwa kuwa kimetokana na kipigo kikali alichokitoa mtuhumiwa dhidi ya mtoto huyo mdogo ambaye alidaiwa kuiba fedha hizo kwa jirani yake ambapo baada ya kipigo hicho mtoto alizirejesha fedha hizo kwa Baba yake mkubwa kama njia ya toba na kujutia kosa la udokozi.

Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Anecletus Malindisa alisema kuwa mtoto huyo alifariki dunia muda mchache wakati anapelekwa katika kituo cha polisi cha kati.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya wazazi Meta.

Vick alikuwa ni mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya Msingi Kambarage iliyopo Jijini Mbeya .


Source: Kalulunga Blogspot

No comments:

Post a Comment