BAO pekee lililofungwa na mshambuliaji Thomas Ulimwengu wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 23, Manyara Stars, limeweza kukipa ushindi kikosi hicho dhidi ya Nigeria kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki Michezo ya Olimpiki itakayofanyika mwakani jijini London, England.
Manyara sasa itahitaji suluhu au sare yoyote katika mchezo wa marudiano utakaopigwa wiki mbili baadaye huko Nigeria ili iweze kusonga mbele katika harakati zake za kushiriki Olimpiki mwakani.
“Watu hawakutarajia kama tutashinda dhidi ya Nigeria ambayo ni timu ngumu kuliko Cameroon, nawapongeza vijana wangu kwa uwezo wao na naahidi kurekebisha kasoro zilizojitokeza katika mechi hii kabla ya kurudiana na wapinzani wetu,” alisema Kocha wa Manyara Stars, Jamhuri Kihwelo mara baada ya mchezo huo.
Ulimwengu alifunga bao hilo kwa shuti kali lililomshinda kipa wa Nigeria, Ajiboye Muniru katika dakika ya 85 akiunganisha krosi safi ya Khamis Mcha.
Ezekiel Kitula - Global Publishers Tz
No comments:
Post a Comment