Monday, June 6, 2011

Inspector apotelewa na Mai Waifu wake


Haruna Kahena ‘Inspector’, amempoteza mkewe, Bahati Shada aliyetoweka nyumbani wanakoishi Tandika, Dar es Salaam akiaga anakwenda kuteka maji bombani. Akizungumza na Ijumaa Wikienda jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Inspector alidai kuwa, mkewe alipotea nyumbani hapo wakati yeye akiwa kwenye kikao cha kuzindua upya kundi lao la Gangwe Mob. “Nilikuwa na washkaji zangu akina Kalama, niliporudi nyumbani majirani waliniambia kuwa, walimuona Bahati akitoka na ndoo ya maji wakadhani anakwenda bombani. “Nimemsubiri hadi sasa hivi tunapochonga ambapo ni saa 3:00 usiku hajarudi nyumbani,” alisema Inspector akionesha kuingiwa na hofu.

No comments:

Post a Comment