
SIYO filamu wala igizo, bali ni tukio la kweli lililozua hekaheka katika Kitongoji cha Shekilango, Ubungo jijini Dar es Salaam.
Wakiwa wanakimbizana, mwanamke akiwa mbele alionekana kushikilia tumbo huku utumbo ukining’inia baada ya kudaiwa kuchomwa kisu na mwanaume huyo.
Mwanamke huyo aliyekuwa akipigania kuinusuru roho yake alikuwa akitoa maneno ya kuomba msaada kutoka kwa wasamaria wema akisema: "Jamani nisaidieni, mume wangu anataka kuniua, anasema nimemsaliti."
Hata hivyo, mwanamke huyo hakuweza kufika mbali kwani alianguka chini na baada ya sekunde chache akatokea mume wake, naye akiwa mtupu huku kisu kikiwa kinamning’inia tumboni baada ya kudaiwa kuwa alijichoma.
Haikuchukua muda mrefu umati wa watu ukafika eneo hilo na kupigwa na bumbuwazi juu ya tukio zima, huku wengine wakisema watu hao walikuwa wamefumaniana.
Muda mfupi baadaye askari wa jeshi la polisi walifika eneo la tukio na kuwachukua watu hao, wakawapeleka katika Kituo cha Polisi cha Urafiki na kufungua jalada la kesi namba URP/ RB/ 5126/2011 Mauaji.
Na Rhobi Chacha - Global Publishers
Click to read more...
No comments:
Post a Comment