
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohammed Shein leo amemteua Ahmed Sheikh Abdulrahman kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya kusimamia usafiri wa baharini Zanzibar.
Taarifa ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Abdulhamid Yahya Mzee amesema uteuzi huo unaanza rasmi kunzia leo Juni 9,2011.
Mwenyekiti huyo wa Bodi aliwahi kuwa Meneja Mkuu wa Zanzibar Wharge na pia Mkurugenzi wa Maeneo huru Zanzibar.
Rais Dk Shein amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa kifungu cha 7(2) cha sheria ya usafiri baharini Zanzibar. Dk Shein pia amemteua Bi.Sharifa Khamis Salim kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Zanzibar.
Dk Shein amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa kifungu cha 7(1) cha sheria ya Baraza la Michezo Zanzibar namba 5 ya mwaka 2010. Bi. Sherifa alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo lililopita.
Uteuzi huo umeanza leo (jana) Juni 9, 2011.
IMETOLEWA NA:
IDARA YA HABARI(MAELEZO) ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment