Wednesday, June 15, 2011

MSANII WA MAIGIZO YA VICHEKESHO 'BAMBO' ANUSURIKA KWENYE AJARI YA BODABODA AVUNJIKA MGUU

MTANGA AKIWA MWENYE MAJONZI MAZITO AKIMTAZAMA SWAHIBA WAKE BAMBO

NDUGU YETU BAMBO AKIWA KITANDANI HUKU AKIWA AMEFUNGWA PIOPI MGUUNI

DEREVA WA PIKI-PIKI ALIYOKUWA AMEPANDA BAMBO, AKIWA KATIKA HALI MBAYA

Mkali wa maigizo ya kuchekesha Bongo, Dickson Samson Makwaya a.k.a Bambo alfajiri ya leo amepata ajali mbaya ya pikipiki na kuvunjika mguu wake wa kulia sehemu ya paja.


Ajali hiyo imetokea eneo la njia panda Kigogo jijini Dar es Salaam ambapo gari aina ya DCM iliigonga pikipiki aliyokodi Bambo wakati akirudi nyumbani kweke. Dereva wa pikipiki aitwae Jumbe Juma kwa sasa hali yake ni mbaya na wote wamelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu.


Source: http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/msanii-bambo-avunjika-mguu-1

No comments:

Post a Comment