Thursday, June 16, 2011

AISHA MADINDA: JAMANI MUNGU MKUBWA

Aisha Mohammed Mbegu ‘Aisha Madinda’ (pichani)amemshukuru Mungu kutokana na kuimarika kwa afya yake baada ya kuzorota kwa muda mrefu.

Mnenguaji huyo ambaye hajaonekana jukwaani kwa kipindi cha miezi mitatu alisema kwa sasa anajisikia vizuri na anachohitaji ni kujipanga ili akipona aweze kutafuta mwanaume wa kuzaa naye.

“Mungu ni mkubwa, siku chache zijazo nitarejea jukwaani kukabiliana na shughuli zangu za kila siku kama zamani,” alisema Aisha.

No comments:

Post a Comment