Mwigizaji mwenye mbwembwe nyingi kutoka ndani ya tasnia ya filamu Bongo Christina Manongi 'Sintah' amemtaka video queen wa Bongo Agness Gerald Masogange kufunga bakuli lake (kunyamza kimya) na kuacha kumapakazia meneno machafu kwenye vyombo vya habari.
Akizungumza na Teentz.com mapema leo Sintah amesema kuwa amesikitishwa sana na kitendo cha Agness kumtaja yeye (Sintah) kuwa ndiye anahusika na kuisambaza kwenye mitandao video inayomuonyesha Agness akiwa mtupu huku pia akionekana kufanaya matendo kadhaa ya kingono.
"Nimemsikia na isitoshe kuna watu wengi wameniambia juu ya hilo la kunitukana na kunitaja redioni kuwa nahusika, mimi sijui lolote awaulize marafiki zake ambao mimi naamini ndiyo wanahusika kuzisambaza kwani hata kwenye BBM yangu ni wao ndiyo walinitumia namuomba afunge bakuli lake la siivyo nitazitoa zaidi kwani ninazo pati wani mpaka 3 na zote nimetumiwa na marafiki zake ambao yeye anacheka nao lakini hajui kama ni ma-sn***ch" alisema Sintah.
Akiendelea zaidi Sintah amefunguka kuwa kamwe hajui lolote kuhusu kamera anayoisma Agnes, kwani binafasi hajawahi kukutana naye na alimjua kupitia nyimbo za wasanii wa Bongo Fleva kwa kuwa msichana huyo anapenda kuuza sura na zaidi hajui hata anapokaa.
STORI NA DISMAS TEN
No comments:
Post a Comment