Thursday, August 2, 2012

MRISHO NGASSA APELEKWA SIMBA SC KWA MKOPO


Kiungo wa Azam FC, Mrisho Ngassa leo amepelekwa Simba SC kwa mkopo na uongozi wa timu yake. Mchezaji huyo aliyekuwa anasadikiwa kutua Yanga SC amepelekwa Simba baada ya pande mbili za Azam FC na Simba SC kufikia makubaliano. Wakati hatua hiyo inachukuliwa, Ngassa mwenyewe anadai hana taarifa yoyote kutoka kwa uongozi wa timu yake ya Azam na wala hajafanya mazungumzo yoyote na Simba. Ngassa amesema kama Azam hawamuitaji ni bora wangekaa naye na kufuata taratibu za kuvunja mkataba kuliko kumpeleka kama mzigo. Mchezaji huyu alikuwa na mkataba na timu hiyo mpaka mwakani.

No comments:

Post a Comment