Monday, August 13, 2012

MBUYU TWITE ATUA RASMI YANGA

Mbuyu Twite (kushoto) akiweka alama ya dole gumba katika mkataba wake mpya wa kuitumikia timu ya Young Africans wiki mbili zilizopita, kulia kwake ni mjumbe wa kamati ya Utendaji Abdallah Bin Kleb.

Mbuyu Twite akiweka saini katika mkataba wake mpaya na timu ya Young Africans.


Mlinzi wa kati wa timu ya APR kutoka nchini Rwanda Mbuyu Twite amekamilisha usajili wake ikiwa ni pamoja na kupata uhamisho wa kimataifa ITC na kuweza kujiunga na mabingwa wa kombe la klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kombe la Kagame timu ya Young Africans Sports Club.

Mbuyu Twite amabye zoezi lake la usajili lilianza takribani wiki mbili zilizopita limefikia mwisho baada ya klabu ya Young Africans kufanikiwa kupata uhamisho wake wa kimataifa kutoka timu aliyokuwa akiichezea ya APR ambapo awali alikuwa akiichezea timu ya st. Lumpopo FC

Twite ambaye alingara sana katika mashindano ya Kagame yaliyomalizika hivi karibuni na Young Africans kuibuka mabingwa, amesema anajisikia furaha na mwenye bahati kufanikiwa kujiunga na mabingwa mara mbili mfululizo wa kombe la Kagame.

Usajili wa Twite ulianza takribani wiki mbili zilizopita ambapo mjumbe wa kamati ya Utendaji wa klabu ya Young Africans Abdallah Bin Kleb aliamua kwenda nchini Rwanda kuhakiksiha zoezi hilo linakamilika haraka ipasavyo, ambapo mara baada ya kumalizana na Twite aliendelea kuhakikisha anafuatilia ITC yake nchini DRC.

Akiongea na www.youngafricans.co.tz Bin Kleb amesema, Young Africans ni timu kubwa katika Ukanda huu, Viongozi wake wanafanya mambo yao kwa uhakika zaidi, hivyo hawakutaka kuongelea suala la Twite mpaka watakapoona wamekamilisha zoezi lote'

"Unajua usajili sio mchezaji kusaini makaratasi ya mkataba tu, kuna kupata barua ya kumruhusu kutoka timu anayotoka, uhamisho wa mchezaji kutoka chama husika cha soka cha nchi, baada ya hapo ndio unaweza kutangaza sasa kwamba ni mchezaji wako halali"alisema Bin Kleb.

Kusajiliwa kwa Mbuyu Twite kunaifanya timu ya Young Africans kuwa na ukuta wa walinzi wa kimataifa akiwemo Kelvin Yondani, Nadir Haroub Cannavaro, Ladislau Mbogo na Ibrahim Job kwa nafasi ya ulinzi wa katikati.

Twite anatarajiwa kuwasili mapema wikii kuungana na wacheji wenzake katika mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara inayotarajiwa kuaanza sepetemba mosi.

Chanzo: YoungAfricansNews

No comments:

Post a Comment