Friday, August 31, 2012

EXCLUSIVE: GADNER G. HABASH AHAMIA RADIO TIMES 100.5 FM

Kapteni Gadner Habash ambaye amejiunga na kituo hicho cha redio na kutangazia umma rasmi akizungumza na wanahabari pamoja na watangazaji wenzake, wanaofuatia katika picha ni Scholastica Mazula, Criford Ndimbo na Dida wa Mchops.
Mtangazaji wa Radio Times 100.5 Scholastica Mazula akizungumza na waandishi wa habari kwenye mgahawa wa City Sports Lounge Posta jijini Dar es Salaam wakati alipomtambulisha rasmi Kapteni Gadner Habash ambaye amejiunga na kituo hicho cha redio hiyo. Hivi karibuni atakuja na kipindi kipya kinachokwenda kwa jina la “Maskani” kitakachozungumzia mambo mbalimbali katika jamii, katika picha kushoto ni Gadner G. Habash mwenyewe na kulia ni Mtangazaji wa kipindi cha michezo Cliford Ndimbo.
Baadhi ya watayarishaji wa vipindi na watangazaji katika redio hiyo wa tatu kutoka kulia ni Mkoloni aliyewahi kuvuma na kundi la Wagosi wa Kaya.
Kapteni Gadner G. Habash kushoto akipozi kwa picha wa mastafu wenzake wapya kutoka kulia ni Dida wa Mchops, Natasha na Scholastica Mazula.

Habari Picha na Haki Ngowi

No comments:

Post a Comment