Monday, August 13, 2012

Dr. Ulimboka arejea nchini tayari kwa kuendeleza mapambano





Dk. Steven Ulimboka amerejea leo nchini bna kutyoa shukrani za dhati kwa watanzania kwa dua na michango yao kuinusuru afya yake na kuahidi kuendeleza mapambano dhidi ya huduma bora za afya na maslahi kwa madaktari.

Ulimboka amerejea nchini wakati jamii bado ikiwa katika kizungu mkuti cha nani hasa aliyemteka na kumpa mateso makali Dk. Steven Ulimboka ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini na kiu ya wananchi sasa ni kutaka kujua ukweli kupitia kwake.

Daktari huyo ambaye amejizolea umaarufu nchini kwa harakati za kudai haki na maslahi ya madkatari na huduma bora Hospitalini amerejea leo jijini Dar es Salaam akitokea nchini Afrika kusini ambako alipelekwa na Madaktari wenzake tangu Juni 30 mwaka ambako alikuwa akitibiwa majeraha aliyoyapata baada ya kutekwa na kundi la watu wasiojulikana.

Dk. Ulimboka alitekwa, kupigwa na kutelekezwa kwenye Msitu wa Pande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam ambapo Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaa lilidai kuwa aliyemteka daktari huyo ni raia wa Kenya ambaye tayari wanamshikilia.

Dk. Ulimboka amewasili leo majiya ya saa 8 alasiri katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na SA Airways na kulakiwa kwa shangwe, hoihoi nderemo na vifijo kutoka kwa ndfugu jamaa na marafiki sambamba na madaktari wenzake na wanaharakati.

Hakika Mungu yupo! Na anatenda miujiza yake, Ulimboka inakumbukwa aliondoka nchini akiwa hajiwezi kutokana na hali yake kuwa mbaya na kubebwa katika machela lakini leo amerejea mzima wa afya na anatembea mwenyewe.


Licha ya vurugu za hapa napale ambazo zilikuwa zikisababishwa na ndugu na jamaa ambao walitaka wanahabari wasilidake tukio hilo la kihistoria mithili ya Mtanzania kutwaa medali ya Dhahabu Olympic 2012 huko London lakini paparaziu waliweza kunasa taswira kadhaa na kuongea nae.

“Nimepona ndugu zangu….nawashukuru nyote mlioniombea, watanzania, madaktari, ndugu na jamaa zangu nashukuru pia kunisaidia kupata matibabu bora hadi leo hii narudi nyumbani, niko fiti nikitembea mwenyewe,” alisema Dk. Ulimboka.

Miongoni mwa wana harakati ambao Father Kidevu Blog ilifanikiwa kuwaona uwanjani hapo ni pamoja na Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Usu Malya na Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari wanawake(TAMWA), Ananileya Nkya.

Wanaharakati hao walijipamba na mabango kadhaa yaliyo kuwa na jumbe za “Dk Ulimboka karibu nyumbani uliumizwa kikatili ukitetea afya bora kwa watanzania.” “Dk Ulimboka damu yako ilimwagika na kuamsha ari kwa wananchi kudai huduma bora za afya.” “Dk Ulimboka wewe ni mpigania haki na afya bora kwa wananchi wote Mungu na watanzania wote tuko nawe.”

Nae Katibu wa Jumuiya hiyo Dk. Edwin Chitage ameiambia father Kidevu Blog kuwa kurejea kwa Dk. Ulimboka akiwa mzima ni ishara ya huduma bora aliyoipata akiwa nje ya nchi.

Usiku wa kuamkia Juni 27, 2012 watu wasiofahamika walimteka, kumpiga, kumng’oa kucha na meno kisha kumtelekeza kwenye msitu wa pande Dk. Ulimboka.

Wakati amelazwa Hospitali ya taifa Muhimbili chumba cha wagonjwa mahututi Kitengo cha Mifupa (MOI) alikuwa akihudumiwa na jopo la madaktari saba akiwapo Profesa Joseph Kahamba.

Licha ya jopo jilo la madaktari kumhudumia kwa ukaribu lakini walishindwa kupata baadhi ya vipimo ili kubaini iwapo damu yake ilikua na sumu ama la kwa kusababu baadhi ya dawa zilishindwa kufanyakazi ndfipo uamuzi wa haraka wa kumpeleka nje ya nchi ukafikiwa na wanachi kumchangia fedha kiasi cha shilingi milioni 40 za matibabu yake.

Aidha Katibu wa Jumuia ya madaktari Dk. Chitage amewaahidi wanahabari kuitisha mkutano mapema ili kujuza umma wa watanzania na dunia kwa kina kuhusu kupona Dk. Ulimboka.

Chanzo: Father Kidevu Blog

No comments:

Post a Comment