Thursday, August 9, 2012

Basi la Sabena lachinja 17 lajeruhi 78 walikuwa zaidi ya 100


WATU 17 wamekufa na wengine 78 kujeruhiwa wilayani Sikonge katika Mkoa wa Tabora baada ya basi la Sabena aina ya Scania lenye namba T570 AAM lililokuwa limejaza kupita kiasi kupata ajali na kupinduka. Basi hilo lilikuw alikitoka tabora kwenda Mbeya.

Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Kitunda wilayani Sikonge umbali wa kilometa 200 kusini mwa mji wa Tabora.

Miongoni wa watu waliokufa ni watoto watano, wanawake sita na wanaume sita na kwamba hadi leo mchana, miili ya watu saba ilikuwa imetambuliwa akiwemo askari Polisi, Konstebo Kheri wa Kituo Kikuu cha Polisi mjini Tabora.

Wengine ni Vitus Tulumanye, Farah Inga (Mzimbabwe), Ikamba Thadeo, Damalu Goma, Beatrice Kalinga , Andrew Madirisha . maiti zilizobaki zipo hospitali ya Kitete zikisubiri utambuzi..

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Antony Ruta, alisema basi hilo lilikuwa limejaa kupita kiasi kwani inaonekana lilikuwa na abiria zaidi ya 100.

CHANZO: http://lukwangule.blogspot.com

No comments:

Post a Comment