RAIS wa Ghana, Evans John Atta Mills (68) amefariki Dunia katika hosipitali moja ya kijeshi iliyopo mji mkuu wa nchi hiyo, Accra.
Mills amekutwa na mauti siku chache tangu aliporejea kutoka Marekani ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Taarifa za mashirika ya habari ya kimataifa zilizotolewa jana jioni zilisema Rais huyo wa tatu wa Ghana aliugua ghafla juzi Jumatatu na alifariki jana mchana baada ya kuzidiwa.
Shirika la Uingereza Reuters lilimnukuu mmoja wa wasadizi wa Rais Mills akisema kuwa rais huyo alikuwa amethibitika kufariki jana mchana.
Habari zaidi zilisema kwa mujibu wa Katiba ya Ghana, Makamu wa Rais John Dramani Mahama alikuwa akitarajiwa kuapishwa jana usiku kuchukua nafasi ya Mills ili kuongoza taratibu za mazishi ya mtangulizi wake.
No comments:
Post a Comment