Wednesday, June 27, 2012

Timu 12 zathibitisha kushiriki Kagame


TIMU 12 zimethibitisha kushiriki michuano ya kuwania Kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Julai 14 hadi 29, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Championi Jumatano jana jijini Dar, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema timu zilizothibitisha kushiriki ni Mafunzo (Zanzibar), APR (Rwanda), Tusker (Kenya), El Mereikh (Sudan), El Man (Somalia) na Ports (Djibouti). Alisema nyingine ni Yanga, Simba, Azam, (Tanzania) Atraco (Burundi), URA (Uganda) na Wausalam (Sudan Kusini).

“Mwisho wa kuthibitisha kushiriki ilikuwa ni Juni 25 na droo ya makundi itachezeshwa Juni 29. “Nchi ambazo mpaka sasa mabingwa wake hawajathibitisha kushiriki ni Eritrea na Ethiopia. Michuano inaanza Julai 14, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa na Chamazi jijini Dar es Salaam,” alisema Wambura.

Na Lucy Mgina, GPL

No comments:

Post a Comment