Friday, June 22, 2012

'MLOKOLE' AMWANGUSHIA MAOMBI USTADHI




KIJANA mmoja anayedaiwa kuwa Mkristo 'Mlokole' na aliyejitambulisha kwa jina moja la Joseph, jana mjini Morogoro alidhihirisha madai hayo baada ya kumvamia jamaa mmoja aitwaye Magari Ramadhani ambaye ni muumini mzuri wa dini ya Kiislam na kumwambia kwamba alikuwa ametumwa kumfanyia maombi.

Hayo yalifanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini hapa ambapo alimtaka muumini huyo kuvua barghashia ili apate nafasi ya kumshika kichwani. Ramadhani alikubali ombi hilo na Joseph akamfanyia maombi, jambo lililowafanya watu waliokuwa jirani kuangua vicheko.

Hata hivyo, habari zilizopatikana baadaye zilidai kwamba kijana huyo ana upugufu wa akili, na Ramadhani naye alipohojiwa alisema anamfahamu kijana huyo kwamba ni mgonjwa wa akili hivyo aliamua kumridhisha na kumpa nafasi ya kumfanyia kile alichoita maombi.

PICHA NA DUNSTAN SHEKIDELE,GPL, MOROGORO

No comments:

Post a Comment