Monday, June 18, 2012

Kaseja: Waongo, bado sijasaini Simba SC


KIPA namba moja wa timu ya taifa, Taifa Stars na Klabu ya Simba, Juma Kaseja, amesema bado hajasaini mkataba mpya wa kuichezea klabu hiyo kama inavyoelezwa.

Kaseja ameitoa kauli hiyo hivi karibuni, baada ya kuwepo taarifa za yeye kusaini mkataba mpya wa kuichezea Simba kufuatia mkataba wake wa awali wa miaka miwili, kumalizika mwezi uliopita.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Kaseja alisema hadi sasa hajasaini popote, hivyo yeye ni mchezaji huru na ana uwezo wa kuondoka kwenda kuichezea timu yoyote.

Kaseja alisema ameshangazwa na taarifa hizo zinazozagaa kuwa amesaini Simba, akidai huo ni uongo na uzushi.

“Ujue hizo taarifa za mimi kusaini mkataba mpya wa kuichezea Simba nimezipata, zimenishangaza sana na nashindwa kuelewa ni nani aliyezusha uongo huo.

“Mimi ni mchezaji huru na bado sijasaini mkataba popote, ni vyema ikajulikana, na kama nikiongeza sitaficha, nitaongea ukweli,” alisema Kaseja.

Na Wilbert Molandi, GPL

No comments:

Post a Comment