Hii ni moja ya msg anazodai Dogo Janja kwamba Madee ndio alikua anajitumia baada ya kumnyanga’nya simu ili kuja uwaonyesha watu kwamba Dogo Janja ndio aliziandika.
Kuna meseji nyingine kadhaa ambazo haziwezi kuwekwa hapa kwa sababu zina matusi sana.
Dogo Janja ambae sasa yuko kwao Arusha aliondoka alhamisi kurudi kwao baada ya kukataa kuendelea kuwa chini ya usimamizi wa Madee akidai kwamba hayakua maisha mazuri, alidhulumiwa kuteswa na hata kutokupata matunzo aliyotakiwa kuyapata.
Akiongea Exclusive kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM Janja alisema kwamba “sitaki kabisa kusoma Dar es salaam nitakwenda kusoma Arusha au mkoa mwingine wowote, alijitumia msg nyingi sana alizoandika kupitia simu yangu ili mimi nionekane mbaya, kuna nyingine aliandika producer Maneke ni snich tu, nyingine mimi nitamloga yani sikuweza kufikiria kwamba mtu mzima wa miaka 32 anaweza kumfanyia kitu kama hicho mtoto wa miaka 16″
Akiongea kwa huzuni baada ya kuulizwa ni kiasi gani cha pesa amewahi kulipwa kutokana na mauzo ya Album yake, Dogo Janja kasema “Eeeeeeehh bro nikizungumzia swala la Album yani daaaaaaahhhhhh, nakumbuka kuna kipindi nilitaka kuliongelea nikawekwa chini nikaambiwa usiliongelee sasa sijui kama ni yule Muhindi au ni Madee, album iliuzwa kwa Muhindi na nilisaini mkataba na kupiga picha za Album ikatoka lakini ile album kiukweli hata ukinipa msaafu sasa hivi nashika, sijawahi kula shilingi tano yangu ya album mi namwachia mwenyenzi Mungu mpaka Madee aliniambia wewe ukiulizwa kwenye Radio sema ile album uliifanya kwa kumbukumbu tu hata ukija kuzeeka utakuja kuwaambia wajukuu zako nilifanyaga album ya Mtoto wa Uswazi ilikua na nyimbo tisa lakini usiitolee macho album haina hela”
“Naapa kwa mwenyenzi Mungu kama nimekula hata shilingi kumi yake nife hata sasa hivi yani, mpaka ilifikia kipindi nikienda kufanya show Mwanza nakwenda kwa Mamu nanunua kopi zangu 20, album niliuza bure mimi nikawa nanunua kwa shilingi elfu mbili pale dukani Umoja, nikifika mikoani ndio nauza CD moja labda shilingi elfu 5 napiga sign watu wanakuja wananunua, kihalali ile Album sikunufaika nayo chochote, wamenufaika nayo watu” – Dogo Janja.
Chanzo: MillardAyoAmplifaya
No comments:
Post a Comment